Nane Nane

Nane Nane

  • Start: Aug 1st, 2020
  • End: Aug 9th, 2020
  • Time: 8:00 AM - 17:00 pm

Maazimisho ya Nane Nane yanayofanyika mkoani simiyu yameanza toka tarehe 01-08-2020. Lengo ni kukutanisha wakulima, wafanyabiashara na wadau wote wa kilimo kuonesha shughuli zote wanazo zifanya ili kuwapa wigo mkubwa wa biashara.

TANECU wakishirikiana na Agripoa wameweza kuhudhuria katika sherehe za maazimisho ya Nane Nane kitaifa kwa ajili ya kuonesha huduma zao.

Mambo wanayoonesha ni pamoja na:-

  1. Uzinduaji wa Tovuti ya TANECU LTD
  2. Uelimishaji juu ya mfumo wa Kanzi data kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu za wakulima kwa lengo la kuwahudumia vyema.

Faida zitakazotokana na Mfumo wa Kanzi Data ni pamoja na:-

Faida watakazo pata wakulima ni pamoja na
1. Kujua eneo mashamba yao yalipo
2. Kujua ukubwa wa mashamba kwa hekari.
3. Kujua umbali toka Chama cha msingi mpaka shambani
4. Kupata Elimu kupitia simu toka kwa wataalamu
5. Kujua madeni wanayodai chama kikuu bila kwenda ofisini (kupitia simu)
6. Kupata habari mbali mbali juu ya kilimo.

Hata hivyo chama pia kitanufaika kwa

1. Kuhudumia wakulima ndani ya muda mfupi
2. Kujua mashamba ya wakulima yalipo pamoja na umiliki halali wa mashamba.
3. Kupanga kwa urahisi juu ya usambazaji wa pembejeo/viatilifu kwa wakulima.
4. Kujua idadi ya wakulima na kujua mahitaji yao ili kuweza kupanga mikakati ya kuwaendeleza wakulima.

Tunawakaribisha wadau mbali mbali pamoja na serikali kuunga mkono juhudi
zetu kwa ajili ya kuwaendeleza wakulima wetu.

Event location

en_USEnglish
en_USEnglish