Serikali imetoa Tsh. Bil 20 kulipa madeni ya wakulima

magu

Serikali imetoa Tsh. Bil 20 kulipa madeni ya wakulima

Serikali imetoa shilling bilioni 20 za kulipa madeni ya wakulima, wasafirishaji, wapuliziaji dawa na waendesha maghala ya korosho. “Rais Magufuli ametoa fedha hizi kwa ajili ya Tandahimba, Masasi, Mtwara na Kibiti kwa ajili ya waliokuwa wamelipwa nusu, waliolipwa kiasi na wasiolipwa kabisa.

Fedha hizi zitaanza kulipwa kesho asubuhi,” Waziri mkuu Kassim Majaliwa ametoa kauli hii leo (Jumapili, Julai 19, 2020) wakati akizungumza na wanachama wa Chama cha Msingi (AMCOS) cha Matogoro na wakazi wa Tandahimba mkoani Mtwara alikoenda kuhamasisha maandalizi ya msimu wa ununuzi wa korosho.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

en_USEnglish
en_USEnglish